PoepiaTAZAMA. GUNDUA. NUNUA.

Msaada

Hela yangu inalindwaje?

Unapolipa, hela haiendi kwa muuzaji mara moja. Poepia inaishikilia salama (escrow) hadi mzigo wako ufike na dirisha la ulinzi la siku 3 limalizike. Ukipata tatizo ndani ya muda huo, unaripoti na hela inabaki imeshikiliwa hadi timu yetu iamue.

Ninalipaje?

Chagua mtandao wako wa simu (M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa) kwenye malipo. Utapokea ombi la malipo kwenye simu yako: weka PIN yako ili kukamilisha. Kama halikuja, bonyeza "Tuma tena" kwenye oda yako.

Mzigo wangu utafika lini?

Muuzaji anaandaa oda, kisha kituo chetu kinapokea na kutuma kwa kundi la usafirishaji la siku hiyo (saa 4 asubuhi, saa 8 mchana au saa 11 jioni). Unaweza kufuatilia kila hatua kwenye ukurasa wa oda, na utaona jina la dereva au basi likishatumwa.

Nikipata tatizo na mzigo?

Fungua oda yako na uguse "Ripoti tatizo" ndani ya siku 3 baada ya kupokea. Eleza kilichotokea. Timu yetu itapitia na unaweza kurudishiwa hela zote au sehemu yake.

Nitarudishiwa hela vipi na lini?

Marejesho yanatumwa kwa mtandao wa simu kwenda kwenye namba ile ile uliyolipa. Utapata ujumbe pale hela inapotumwa kweli.

Ninawezaje kufuta oda?

Unaweza kufuta oda kabla ya kulipa, au baada ya kulipa mradi muuzaji hajaanza kuiandaa. Ukilipa, hela inarudishwa yenyewe.

Ninawezaje kufuta akaunti yangu?

Nenda Wasifu > Futa akaunti. Akaunti inafungwa mara moja na taarifa zako binafsi hufutwa baada ya siku 30.

Bado unahitaji msaada?